Hii
ni bahati ya mtende kuota jangwani! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatajwa rais pekee anayetoa sapoti
kwa wasanii ambapo safari hii amempa ulaji staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ishu hiyo
ilitokea mwanzoni mwa wiki baada ya kukutana jijini New York, Marekani
huku kila mmoja akiwa na majukumu yake kwenye ardhi hiyo ya Rais Barrack
Obama.
Ilisemekana kwamba JK kamkutanisha Diamond na meneja wa staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani, Trey Songz.
Kuna madai
kuwa lengo la kumkutanisha Diamond na jamaa huyo ni ili afanye kolabo
na Trey Songz hivyo kumweka kimataifa zaidi kama ilivyo kwa P-Squire.
Ilisemekana kwamba kama kolabo hiyo itafanikiwa JK atakuwa ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.
Ilisemekana kwamba kama kolabo hiyo itafanikiwa JK atakuwa ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.
Staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. akiwa kwenye meza moja
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Stori hiyo iliambatana na picha zilizomuonesha JK akiwa karibu na meneja wa Trey Songz huku Diamond akiwasikiliza kwa umakini.
Ilisemekana JK alizungumza na wasanii hao kwa muda mrefu katika mazungumzo ambayo yalionekana mazito.
Habari zilieleza kuwa JK alifanya hivyo kwa sababu siku zote amekuwa akitoa sapoti kubwa kwa wasanii wake wa Tanzania.
Baada ya
Diamond kukutana na JK kwenye kikao hicho kizito na meneja wa Trey
Songz, Diamond aliandika kwenye kurasa zake za kijamii:
“Wapi
utapata rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao
unatafutwa karibu na kila mtu duniani…akautumia kukusaidia kukukutanisha
na kuku-connect na mdau mkubwa duniani katika tasnia uliyopo ili
kuhakikisha tu unafikia malengo na ndoto ya kazi zako….
“Dah! Asante sana mh. rais, Mwenyezi Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za maisha yako.”
No comments:
Post a Comment