Kwa Tanzania tumeanza kuona matunda ya muziki wa Bongo Flava kipindi
hiki kwa kuzingatia kuwa mwanzoni watu walikuwa wanalipwa hadi 50,000
kwa show moja lakini sasa wasanii wanachukua hata zaidi ya milioni 5 kwa
show ya ndani.
Huko
Nigeria watu wanaowekeza kwenye muziki wameanza kuyaona matunda yao
hivi sasa ambapo kaka yake Davido ambaye pia ni mmiliki wa label HKN
record akiwa na Davido ameweka wazi kuwa Davido huingiza $50,000 (zaidi
ya Milioni 84) kwa show moja anayofanya.
Anasema aliwekeza kiasi cha $50,000 katika label hiyo awali na sasa Davido anapiga kiasi hicho kwa show moja tu.
Davido ni mshindi wa tuzo mbili za MTV MAMA 2014.
No comments:
Post a Comment