Kwa muda mrefu mkali wa Ilala, Chid Benz aka Chuma amekuwa kimya
kwenye game na mwaka huu ameamua kurudi tena na ujio mpya
unaowakutanisha wasanii wa Tanzania wanaoheshimika kwenye level za
kimataifa, AY na Diamond Platinumz.
Chid amepiga story na sammisago.com exclusively na kuuelezea mfumo wa ngoma yake mpya aliyofanya na wakali hao.
Amesema ni ngoma kali yenye verse 3 ambapo yeye anasimama kwenye verse mbili, AY anainyonga verse halafu mtoto wa Tandale, Platinumz amefanya yake kwenye kiitikio na kibwagizo.
Wimbo huo umetayarishwa na producers watatu, Dully Sykes amefanya mdundo kwa mara ya kwanza halafu mixing na vocal zimekamilishwa na Tud Thomas na Emma The Boy.
Lakini jina na tarehe za kuachiwa wimbo huo bado hazijakua wazi. Endelea kutembelea omaryramsey.blogspot.com uwe wa kwanza kuusikia wimbo na chochote kutoka kwa Chuma Chid Benz.
Chid ameshare picha mpya kwenye Instagram kuashiria ujio wake:

No comments:
Post a Comment