Kwa muda mrefu wafuasi wa mwanamuziki
Ally Salehe Kiba maarufu Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu
zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa kando ya muziki kwa muda mrefu.
Alikiba ambaye aliachia wimbo wake wa mwisho “My Everything” Novemba
2012 hajawahi kuachia tena wimbo mwingine, licha ya kutoa kazi kadhaa
alizokuwa akishirikishwa na mdogo wake msanii Abdu Kiba ukiwamo
“Kidela”.
Starehe ilikaa kitako na msanii huyu
aliyewahi kutamba na wimbo wake wa kwanza “Sinderela” mwaka 2007,
nyumbani kwake Kunduchi Beach na ambapo aliainisha mambo makubwa matatu
yaliyomfanya asimame kwa muda kuachia kazi za muziki.
Anasema familia yake ni kitu chenye uthamani mkubwa kwake ndiyo maana alijitoa ili kuhakikisha inakaa sawa.
Jambo la tatu analifafanua kuwa
ilimchukua muda kufikiria namna atakavyowaacha wasanii wengine Tanzania,
na wao wajulikane ndani na nje ya nchi.
Anasema kwa kipindi cha miaka mitatu
aliyopumzika, amejifunza mengi na pia ameona kumekuwa na mapungufu
katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya na maendeleo pia.
“Mapungufu yamekuwepo, lakini kuna
mafanikio mengi pia, kuna baadhi ya wasanii wamefanikiwa kufanya muziki
mzuri na kuutangaza kimataifa na wengine wametengeneza kazi nzuri,
lakini kinachonitisha ladha ya muziki wetu asili hasa ya bongofleva,
imepotea tumeanza kutengeneza muziki wenye utofauti mkubwa sana na
kipindi cha nyuma, kwa kuiga ala ya muziki wa Nigeria na mataifa
mengine,” anasema Alikiba.
Albamu mbili, singo mpya wiki ijayo
Alikiba aliyetamba na wimbo “Dushelele”
miaka miwili iliyopita, ameweka wazi ujio wake wiki ijayo akiwa chini ya
kampuni kubwa barani Afrika ambayo hajataka kuiweka wazi, anasema
alikuwa ‘chimbo’ kwa takribani miaka miwili akiandaa kazi mpya ambapo
amefanikiwa kukamilisha albamu mbili na punde kuachia singo mpya.
Credit By OmaryRamsey
No comments:
Post a Comment