Monday, 19 May 2014

Mwana FA: Mfalme inaongea ukweli, Video kufanyika.. (News)



Baada ya kuachia ngoma ya Mfalme ambayo mitaa imeielewa kwa kiasi kikubwa, Mwana FA ameweka wazi kuwa, wazo la kusuka ngoma hii ni kuweka wazi mambo yanayoizunguka jamii, kuikumbusha kuwa kadri kila mtu anavyojiona kuwa hana, kuna ambao hawana zaidi.

Mwana FA pia amefunguka kuwa, kutokana na kupenda kufanya muziki mzuri, anafeel sana muziki wa G Nako na pia alikuwa na mipango ya siku nyingi ya kufanya kazi na Nahreel ili kutengeneza muunganiko ambao watu watauelewa zaidi.

Kuhusiana na mipango ya video ya kazi hii, Mwana FA akatuchana kuwa mipango imeshapangika, na ndani ya wiki hizi mbili watasafiri kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kwaajili ya kufanya kazi hii ambayo amepewa Director Kelvin Bosco Jr.

No comments:

Post a Comment