Friday 8 September 2017

Makala: Mameneja hawa wa kike ni shiida!!




Inaweza kuwa ni nadra kusikia katika Tasnia ya Muziki au Filamu kuwepo na mameneja wa kike (wanawake), ambao wanaweza kusimama na kufanya mautundu yao, ubunifu pamoja na kutoa fedha ili wasanii wanaowasimamia wafanye vizuri na kuwa gumzo Bongo.

Ni kweli suala hili Kibongobongo bado ni mtambuka, yaani wapo wachache lakini waliopo, wanafanya mambo mengi makubwa kuliko wengi wanavyodhani.

Seven Mosha

Jina lake la kwenye paspoti ni Christine Mosha, amezaliwa Nairobi Kenya, lakini akiwa na miaka minne wazazi wake walihamia mkoani Kilimanjaro, Tanzania.

Baada ya kufundishwa juu ya maajabu saba ya dunia, mwanadada huyo ambaye aliwahi kufanya kazi katika Kituo cha Redio cha Clouds FM kabla ya kujiunga na MTV mwaka 2010, kisha Sony Music, aliamua kubadilisha jina na kujiita Seven Mosha!

Kwa sasa ndiye msimamizi wa lebo ya muziki ya Rockstar4000 na meneja wa mkali wa Ngoma ya Seduce Me, Ali Kiba.

Seven alikutana na Ali Kiba katika ‘project’ ya One8, ambapo yeye alikuwa na jukumu la kusimamia wasanii kutoka Afrika Mashariki.

Mwanadada huyu amefanya kazi na Ali Kiba kwa muda wa miaka sita mpaka sasa na Gazeti la Daily Nation linamuita Malkia wa Marejeo (Queen Of Comebacks), kutokana na kitendo cha kuwarudisha kwenye gemu Ali Kiba na project ya Mwana na Lady Jaydee na Ngoma ya Ndindindi baada ya kuwa wamepotea. Lakini pia amewahi kumsimamia Barakah The Prince.

Lamata

Ni mtunzi na muongozaji wa filamu maarufu Bongo. Miongoni mwa filamu alizoo-ngoza ni The Safety Catch pamoja na Candy iliyochezwa na Jacqueline Wolper.

Jina lake halisi ni Leah Mwendamseke na meneja wa wasanii wa filamu Bongo. Wasanii ambao ameshawahi kuwasimamia kwa mafanikio makubwa ni Jacquline Wolper pamoja na Kajala Masanja.
Kwa sasa bado anamsimamia Kajala akiwa pia na Asha Boko na Tausi.

Neema Ndepanya

Huyu ndiye kila kitu kwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu a.k.a ‘Tanzania Sweetheart’ kwa sasa.
Ukipenda unaweza kumuita ‘bodigadi’ au meneja yote kwake ni sawa tu lakini kwa jumla ndiye mtu wa karibu ambaye anasimamia ‘project’ pamoja na mambo mengi kwenye maisha binafsi ya mrembo huyo.

Kama ilivyo kwa Lamata, Neema pia ni mtunzi muongozaji na muigizaji mwenye jina Bongo. Ameshiriki kwenye filamu za Utamu Wangu, Kivuruge na ndiye aliyeongoza muvi mpya ya Wema Sepetu iitwayo Heaven Sent.

Kwa sasa anabaki kuwa kama meneja na msimamizi wa kazi za filamu za Wema.

Irene Sabuka

Kwa watu wanaofuatilia burudani ya muziki Bongo jina la Harmorapa si geni kabisa. Ukweli ni kwamba si ngoma za Usigawe Pasi, Kiboko ya Mabishoo au Nundu ndizo zimemuweka kwenye ramani ya muziki pekee, bali kujua fitna ya muziki, utundu pamoja na pesa za mwanadada huyu ndizo zimemuweka kwenye ramani ya muziki Harmorapa.

Irene Sabuka anaingia kwenye orodha hii akiwa ni mwanamke wa shoka ambaye pia anaelea kwenye ulimwengu wa burudani akiwa msimamizi za kazi za wasanii.

Muna

Anaingia katika listi hii akiwa naye ni mmoja kati ya mameneja kwenye muziki akiwa amejitosa kwenye Muziki wa Singeli.

Ikumbukwe kuwa ndiye aliyemfanya Sholo Mwamba akasimama vizuri huku akisimamia project zake na shoo zake kibao za ndani kupitia kampuni yake ya Muna Logistic akishirikiana na kampuni ya Wema ya Endless Fame.

Kwa sasa bado anaendelea kusimamia kazi za wasanii.

No comments:

Post a Comment