Monday 3 July 2017

Dj Khaled ashika namba moja Billboard


Albamu ya mtayarishaji wa muziki Dj Khaled imeshika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 200 kwa mara ya kwanza tangu alipoachia albamu hiyo inayoitwa ‘GRATEFUL’ tarehe 23 mwezi Juni.

Hii ni albamu ya pili ya Dj Khaled kufika namba moja kwenye chati za Billboard baada ya albamu yake ya Major Key kufanya hivyo tarehe 20 mwezi Agosti mwaka 2016.

Billboard Hot 200 hupanga chati za albamu bora zilizotoka ndani ya wiki moja kulingana na mauzo ya ndani na nje ya nchi pia mauzo ya mtandaoni ya iTunes Store kupitia Apple Music.

No comments:

Post a Comment