Thursday 3 September 2015

Sasa historia ya maisha ya drogba kupatikana kwenye kitabu hiki “Commitment“

Drogba ni mmoja wa mastaa wakubwa Afrika na hata soka la Ulaya, Novemba mwaka huu anatarajia kuzindua kitabu kitakachozungumzia maisha yake kwa ujumla.

Akiwa na miaka yake 37 mshambuliaji huyo ameahidi kutoa kitabu hicho ambacho kitazungumzia pia na maisha yake akiwa Ufaransa, umuhimu wa elimu, jinsi ya kutafuta mafanikio katika maisha.

Pia kitazungumzia maisha yake ya kawaida na ya nje ya uwanja hasa akiwa na klabu yake ya Chelsea. Kitabu hicho kitabeba jina la “Commitment“.


Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya


No comments:

Post a Comment