Thursday, 27 August 2015

P-Square wavunja rekodi tena kwa video yao ‘Personally’ kuwa ya kwanza Afrika kufikisha views M50 Youtube

Kundi La P Square limeingia kwenye rekodi mpya baada ya video ya ngoma yao ya ‘Personally’ kufikisha views milioni 50 kupitia mtandao wa YouTube.

Video hiyo iliyotoka mwaka 2013 imekuwa Video ya kwanza Afrika kufikisha idadi ya watu wengi zaidi waliyoitazama ambayo ilisimamiwa na kaka yao Jude Okoye.


November 2014, P-Square waliweka rekodi kwa mara ya kwanza kwa kuwa wasanii wa kwanza Afrika kufikisha views milioni 30 Youtube kupitia video hiyo.

April 2015 kundi hilo lilivunja tena rekodi yao wenyewe baada ya video hiyo kufikisha views milioni 40.

Na sasa tena video hiyo iliyotoka June 21, 2013 imekuwa video ya kwanza ya msanii wa Afrika kufikisha zaidi ya views milioni 50. Video ya ‘Personally’ iliongozwa na kaka yao Jude Engees Okoye.

Jikumbushie kwa kuitazama hapo juu

Jiunge Nasi na Huku Pia, Kwa Kubofya



No comments:

Post a Comment